Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Ali Khomeini katika mahojiano yaliyotangazwa Jumatano usiku na mtandao wa habari wa Al-Mayadeen, alitangaza kuwa; anaona mustakabali wa Mapinduzi ya Kiislamu kuwa mzuri, na kwamba njia pekee ya maisha katika ulimwengu ambao Marekani na Israeli wameugeuza kuwa kama msitu ni muqawama, na kwamba Iran kwa sasa iko katika mapambano ya kimaumbile ya kuwepo kwake.
Alisema kuwa lengo la utawala wa Kizayuni katika vita dhidi ya Iran ni “kuivunja Iran tu”, na akaongeza kuwa; utawala huo ni kituo kikuu cha Marekani katika eneo hili. Alisema mataifa ya Kiislamu yakipata uwezo, yataifanyia Israeli yale ambayo Hamas ilifanya tarehe 7 Oktoba 2023.
Mjukuu wa Imam Khomeini (r.a) aliongeza kuwa: “Uchambuzi wangu ni kwamba vita kati ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ni jambo lililo mbali sana kutokea. Lakini kama vita vitatokea, hatutaogopa na tutavikabili, na tayari tumethibitisha uwezo wetu.”
Alisisitiza kuwa; Wamarekani na Waisraeli wameonesha kuwa dunia imekuwa kama msitu, na kutofautisha kati ya Waisraeli na Wamarekani — hata kama inawezekana — hakuna maana.
Akijibu swali kuhusu mustakabali wa mapinduzi, alisema: Ndiyo, kuna wasiwasi, lakini hakuna hofu. Wasiwasi ni jambo la kawaida, kwa sababu mtu akipenda kitu na akaona kinatishiwa kuangamizwa, moyo wake huingiwa na wasiwasi. Lakini hofu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu — hapana.
Njia hii tuliyoichagua, mwanzo wake ni kujitoa mhanga na mwisho wake ni shahada, na ndani yake hakuna kushindwa.
Aliendelea kusema: “Njia pekee ya maisha yetu ni muqawama, na sasa tuko katika vita vya kuwepo. Marekani imeweka mshirika wake wa kimkakati katika eneo hili — Israeli.
Israeli inajua kuwa siku mataifa ya Kiislamu yatakapoweza kuishambulia, yatafanya hivyo. Leo baadhi ya nchi hazitekelezi wajibu huo kwa sababu hazina uwezo.”
Aliendelea kusema kwamba: “Sera ya uhakika ya Marekani na Israeli ni kudhoofisha eneo hili. Israeli, ikipata uwezo, itazuia fursa za kiuchumi za nchi za Kiislamu.
Tuko katika vita. Israeli inalenga kuivunja na kuidhoofisha Iran, kama ilivyofanywa kwa Dola ya Ottoman. Iwapo Iran kubwa itageuzwa kuwa nchi ndogo ndogo, nchi hizo zitahitaji washirika — na hapo Israeli itatoa amri na wao watalazimika kutii.”
Aliongeza kuwa; uamuzi wa kuchagua muqawama ulitokana na uono wa uhalisia. Imam Khomeini alikuwa mtu wa dini lakini pia mtu wa uhalisia. Leo pia Jamhuri ya Kiislamu inaangalia mambo kwa uhalisia huo.
Alisema: Marekani imeichagua Israeli kuwa mshirika wake, na kuitofautisha Marekani na Israeli hakuna maana, kwa sababu Israeli ni kituo kikubwa zaidi cha kijeshi cha Marekani katika eneo hili.
Alisema kuwa mabeberu huzungumza kwa lugha ya nguvu, na kwa lugha hiyo hiyo inaweza kukabiliwa. Akaongeza kuwa miezi michache iliyopita Iran ilifanya hatua tatu: kurusha makombora, kufikia malengo na kusababisha uharibifu. Na kila moja ingetosha kufanya taifa lipendwe na Waislamu.
Sayyid Ali Khomeini alisema kuwa: “Kwa mujibu wa tafiti za maoni, leo Ayatullah Khamenei ndiye mtu maarufu zaidi na mwenye nguvu zaidi Iran. Anaunganisha nguvu na umaarufu.”
Maoni yako